بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
سَبِّحِ ٱسْمَ رَبِّكَ ٱلْأَعْلَى ﴿١﴾
87:1 Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
ٱلَّذِى خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾
87:2 Aliye umba, na akaweka sawa,
وَٱلَّذِى قَدَّرَ فَهَدَىٰ ﴿٣﴾
87:3 Na ambaye amekadiria na akaongoa,
وَٱلَّذِىٓ أَخْرَجَ ٱلْمَرْعَىٰ ﴿٤﴾
87:4 Na aliye otesha malisho,
فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحْوَىٰ ﴿٥﴾
87:5 Kisha akayafanya makavu, meusi.
سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ ﴿٦﴾
87:6 Tutakusomesha wala hutasahau,
إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّهُۥ يَعْلَمُ ٱلْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ ﴿٧﴾
87:7 Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٨﴾
87:8 Na tutakusahilishia yawe mepesi.
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكْرَىٰ ﴿٩﴾
87:9 Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ ﴿١٠﴾
87:10 Atakumbuka mwenye kuogopa.
وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلْأَشْقَى ﴿١١﴾
87:11 Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
ٱلَّذِى يَصْلَى ٱلنَّارَ ٱلْكُبْرَىٰ ﴿١٢﴾
87:12 Ambaye atauingia Moto mkubwa.
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿١٣﴾
87:13 Tena humo hatakufa wala hawi hai.
قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ﴿١٤﴾
87:14 Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
وَذَكَرَ ٱسْمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ ﴿١٥﴾
87:15 Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
بَلْ تُؤْثِرُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا ﴿١٦﴾
87:16 Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
وَٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰٓ ﴿١٧﴾
87:17 Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
إِنَّ هَـٰذَا لَفِى ٱلصُّحُفِ ٱلْأُولَىٰ ﴿١٨﴾
87:18 Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
صُحُفِ إِبْرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾
87:19 Vitabu vya Ibrahimu na Musa.