بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتْ ﴿١﴾
82:1 Mbingu itapo chanika,
وَإِذَا ٱلْكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتْ ﴿٢﴾
82:2 Na nyota zitapo tawanyika,
وَإِذَا ٱلْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾
82:3 Na bahari zitakapo pasuliwa,
وَإِذَا ٱلْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾
82:4 Na makaburi yatapo fukuliwa,
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾
82:5 Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَـٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلْكَرِيمِ ﴿٦﴾
82:6 Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?
ٱلَّذِى خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾
82:7 Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,
فِىٓ أَىِّ صُورَةٍ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ ﴿٨﴾
82:8 Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.
كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ ﴿٩﴾
82:9 Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَـٰفِظِينَ ﴿١٠﴾
82:10 Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,
كِرَامًا كَـٰتِبِينَ ﴿١١﴾
82:11 Waandishi wenye hishima,
يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾
82:12 Wanayajua mnayo yatenda.
إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍ ﴿١٣﴾
82:13 Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,
وَإِنَّ ٱلْفُجَّارَ لَفِى جَحِيمٍ ﴿١٤﴾
82:14 Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ ٱلدِّينِ ﴿١٥﴾
82:15 Wataingia humo Siku ya Malipo.
وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَآئِبِينَ ﴿١٦﴾
82:16 Na hawatoacha kuwamo humo.
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ ﴿١٧﴾
82:17 Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
ثُمَّ مَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ ﴿١٨﴾
82:18 Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْـًٔا ۖ وَٱلْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّهِ ﴿١٩﴾
82:19 Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.