بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱلرَّحْمَـٰنُ ﴿١﴾
55:1 Arrah'man, Mwingi wa Rehema
عَلَّمَ ٱلْقُرْءَانَ ﴿٢﴾
55:2 Amefundisha Qur'ani.
خَلَقَ ٱلْإِنسَـٰنَ ﴿٣﴾
55:3 Amemuumba mwanaadamu,
عَلَّمَهُ ٱلْبَيَانَ ﴿٤﴾
55:4 Akamfundisha kubaini.
ٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ ﴿٥﴾
55:5 Jua na mwezi huenda kwa hisabu.
وَٱلنَّجْمُ وَٱلشَّجَرُ يَسْجُدَانِ ﴿٦﴾
55:6 Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
وَٱلسَّمَآءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ ٱلْمِيزَانَ ﴿٧﴾
55:7 Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani,
أَلَّا تَطْغَوْا۟ فِى ٱلْمِيزَانِ ﴿٨﴾
55:8 Ili msidhulumu katika mizani.
وَأَقِيمُوا۟ ٱلْوَزْنَ بِٱلْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا۟ ٱلْمِيزَانَ ﴿٩﴾
55:9 Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.
وَٱلْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ ﴿١٠﴾
55:10 Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
فِيهَا فَـٰكِهَةٌ وَٱلنَّخْلُ ذَاتُ ٱلْأَكْمَامِ ﴿١١﴾
55:11 Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
وَٱلْحَبُّ ذُو ٱلْعَصْفِ وَٱلرَّيْحَانُ ﴿١٢﴾
55:12 Na nafaka zenye makapi, na rehani.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٣﴾
55:13 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
خَلَقَ ٱلْإِنسَـٰنَ مِن صَلْصَـٰلٍ كَٱلْفَخَّارِ ﴿١٤﴾
55:14 Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..
وَخَلَقَ ٱلْجَآنَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ ﴿١٥﴾
55:15 Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٦﴾
55:16 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
رَبُّ ٱلْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ ٱلْمَغْرِبَيْنِ ﴿١٧﴾
55:17 Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٨﴾
55:18 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
مَرَجَ ٱلْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ ﴿١٩﴾
55:19 Anaziendesha bahari mbili zikutane;
بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ ﴿٢٠﴾
55:20 Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢١﴾
55:21 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يَخْرُجُ مِنْهُمَا ٱللُّؤْلُؤُ وَٱلْمَرْجَانُ ﴿٢٢﴾
55:22 Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٣﴾
55:23 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
وَلَهُ ٱلْجَوَارِ ٱلْمُنشَـَٔاتُ فِى ٱلْبَحْرِ كَٱلْأَعْلَـٰمِ ﴿٢٤﴾
55:24 Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٥﴾
55:25 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾
55:26 Kila kilioko juu yake kitatoweka.
وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو ٱلْجَلَـٰلِ وَٱلْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾
55:27 Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٨﴾
55:28 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يَسْـَٔلُهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِى شَأْنٍ ﴿٢٩﴾
55:29 Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٠﴾
55:30 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ ٱلثَّقَلَانِ ﴿٣١﴾
55:31 Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٢﴾
55:32 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يَـٰمَعْشَرَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ إِنِ ٱسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا۟ مِنْ أَقْطَارِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ فَٱنفُذُوا۟ ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَـٰنٍ ﴿٣٣﴾
55:33 Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٤﴾
55:34 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ ﴿٣٥﴾
55:35 Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٦﴾
55:36 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فَإِذَا ٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَٱلدِّهَانِ ﴿٣٧﴾
55:37 Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٨﴾
55:38 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْـَٔلُ عَن ذَنۢبِهِۦٓ إِنسٌ وَلَا جَآنٌّ ﴿٣٩﴾
55:39 Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٠﴾
55:40 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يُعْرَفُ ٱلْمُجْرِمُونَ بِسِيمَـٰهُمْ فَيُؤْخَذُ بِٱلنَّوَٰصِى وَٱلْأَقْدَامِ ﴿٤١﴾
55:41 Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٢﴾
55:42 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
هَـٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِى يُكَذِّبُ بِهَا ٱلْمُجْرِمُونَ ﴿٤٣﴾
55:43 Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ ءَانٍ ﴿٤٤﴾
55:44 Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٥﴾
55:45 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ جَنَّتَانِ ﴿٤٦﴾
55:46 Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٧﴾
55:47 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
ذَوَاتَآ أَفْنَانٍ ﴿٤٨﴾
55:48 Bustani zenye matawi yaliyo tanda.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٩﴾
55:49 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ ﴿٥٠﴾
55:50 Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥١﴾
55:51 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِمَا مِن كُلِّ فَـٰكِهَةٍ زَوْجَانِ ﴿٥٢﴾
55:52 Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٣﴾
55:53 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ فُرُشٍۭ بَطَآئِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى ٱلْجَنَّتَيْنِ دَانٍ ﴿٥٤﴾
55:54 Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٥﴾
55:55 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِنَّ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَآنٌّ ﴿٥٦﴾
55:56 Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٧﴾
55:57 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
كَأَنَّهُنَّ ٱلْيَاقُوتُ وَٱلْمَرْجَانُ ﴿٥٨﴾
55:58 Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٩﴾
55:59 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
هَلْ جَزَآءُ ٱلْإِحْسَـٰنِ إِلَّا ٱلْإِحْسَـٰنُ ﴿٦٠﴾
55:60 Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦١﴾
55:61 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ ﴿٦٢﴾
55:62 Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٣﴾
55:63 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
مُدْهَآمَّتَانِ ﴿٦٤﴾
55:64 Za kijani kibivu.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٥﴾
55:65 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ ﴿٦٦﴾
55:66 Na chemchem mbili zinazo furika.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٧﴾
55:67 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِمَا فَـٰكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ ﴿٦٨﴾
55:68 Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٩﴾
55:69 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِنَّ خَيْرَٰتٌ حِسَانٌ ﴿٧٠﴾
55:70 Humo wamo wanawake wema wazuri.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧١﴾
55:71 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
حُورٌ مَّقْصُورَٰتٌ فِى ٱلْخِيَامِ ﴿٧٢﴾
55:72 Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٣﴾
55:73 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَآنٌّ ﴿٧٤﴾
55:74 Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٥﴾
55:75 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِىٍّ حِسَانٍ ﴿٧٦﴾
55:76 Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri.
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٧﴾
55:77 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
تَبَـٰرَكَ ٱسْمُ رَبِّكَ ذِى ٱلْجَلَـٰلِ وَٱلْإِكْرَامِ ﴿٧٨﴾
55:78 Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.