QuranQuiz bySALSABIL STUDIO
Open the appOpen app

سورة الصافات

Surat As-Saffat kwa Kiswahili

Aya 182 · Sura ya 37 kati ya 114

🌐 Translation: Kiswahili

Englishالعربية (بلا ترجمة)اردوBahasa IndonesiaBahasa MelayuTürkçeFrançaisDeutschEspañolPortuguêsItalianoNederlandsРусскийفارسیবাংলাहिन्दीSoomaaliKiswahiliHausaShqipBosanskiAzərbaycancaOʻzbekcha中文日本語한국어ภาษาไทยTiếng ViệtTagalogپښتوPolskiSvenskaNorskSuomiČeštinaRomânăБългарскиУкраїнськаעבריתதமிழ்മലയാളംతెలుగుमराठीગુજરાતીनेपालीසිංහලঅসমীয়াسنڌيدریKurdîދިވެހިئۇيغۇرچەአማርኛAfaan OromooYorùbáKinyarwandaBamanankanChiyaoTamaziɣtMëranawТоҷикӣҚазақшаТатарчаភាសាខ្មែរEnglish (Abdel Haleem)

Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلصَّـٰٓفَّـٰتِ صَفًّا ﴿١﴾

37:1 Naapa kwa wanao jipanga kwa safu.

فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجْرًا ﴿٢﴾

37:2 Na kwa wenye kukataza mabaya.

فَٱلتَّـٰلِيَـٰتِ ذِكْرًا ﴿٣﴾

37:3 Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.

إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَٰحِدٌ ﴿٤﴾

37:4 Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.

رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ ٱلْمَشَـٰرِقِ ﴿٥﴾

37:5 Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.

إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِزِينَةٍ ٱلْكَوَاكِبِ ﴿٦﴾

37:6 Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.

وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَـٰنٍ مَّارِدٍ ﴿٧﴾

37:7 Na kulinda na kila shet'ani a'si.

لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ ﴿٨﴾

37:8 Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.

دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ ﴿٩﴾

37:9 Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.

إِلَّا مَنْ خَطِفَ ٱلْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُۥ شِهَابٌ ثَاقِبٌ ﴿١٠﴾

37:10 Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara.

فَٱسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَآ ۚ إِنَّا خَلَقْنَـٰهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍۭ ﴿١١﴾

37:11 Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata.

بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ ﴿١٢﴾

37:12 Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.

وَإِذَا ذُكِّرُوا۟ لَا يَذْكُرُونَ ﴿١٣﴾

37:13 Na wanapo kumbushwa hawakumbuki.

وَإِذَا رَأَوْا۟ ءَايَةً يَسْتَسْخِرُونَ ﴿١٤﴾

37:14 Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara.

وَقَالُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

37:15 Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.

أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿١٦﴾

37:16 Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلْأَوَّلُونَ ﴿١٧﴾

37:17 Hata baba zetu wa zamani?

قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَٰخِرُونَ ﴿١٨﴾

37:18 Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.

فَإِنَّمَا هِىَ زَجْرَةٌ وَٰحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ ﴿١٩﴾

37:19 Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!

وَقَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ ٱلدِّينِ ﴿٢٠﴾

37:20 Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.

هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ ﴿٢١﴾

37:21 Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.

۞ ٱحْشُرُوا۟ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ وَأَزْوَٰجَهُمْ وَمَا كَانُوا۟ يَعْبُدُونَ ﴿٢٢﴾

37:22 Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu -

مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْجَحِيمِ ﴿٢٣﴾

37:23 Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!

وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْـُٔولُونَ ﴿٢٤﴾

37:24 Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:

مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ ﴿٢٥﴾

37:25 Mna nini? Mbona hamsaidiani?

بَلْ هُمُ ٱلْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ ﴿٢٦﴾

37:26 Bali hii leo, watasalimu amri.

وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ ﴿٢٧﴾

37:27 Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.

قَالُوٓا۟ إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ ٱلْيَمِينِ ﴿٢٨﴾

37:28 Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.

قَالُوا۟ بَل لَّمْ تَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ ﴿٢٩﴾

37:29 Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.

وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَـٰنٍۭ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَـٰغِينَ ﴿٣٠﴾

37:30 Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.

فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَآ ۖ إِنَّا لَذَآئِقُونَ ﴿٣١﴾

37:31 Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.

فَأَغْوَيْنَـٰكُمْ إِنَّا كُنَّا غَـٰوِينَ ﴿٣٢﴾

37:32 Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.

فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِى ٱلْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ ﴿٣٣﴾

37:33 Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ ﴿٣٤﴾

37:34 Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu.

إِنَّهُمْ كَانُوٓا۟ إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾

37:35 Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna.

وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓا۟ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍۭ ﴿٣٦﴾

37:36 Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?

بَلْ جَآءَ بِٱلْحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلْمُرْسَلِينَ ﴿٣٧﴾

37:37 Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume.

إِنَّكُمْ لَذَآئِقُوا۟ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَلِيمِ ﴿٣٨﴾

37:38 Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.

وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٣٩﴾

37:39 Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ ﴿٤٠﴾

37:40 Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.

أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ ﴿٤١﴾

37:41 Hao ndio watakao pata riziki maalumu,

فَوَٰكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ ﴿٤٢﴾

37:42 Matunda, nao watahishimiwa.

فِى جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ ﴿٤٣﴾

37:43 Katika Bustani za neema.

عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَـٰبِلِينَ ﴿٤٤﴾

37:44 Wako juu ya viti wamekabiliana.

يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍۭ ﴿٤٥﴾

37:45 Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem

بَيْضَآءَ لَذَّةٍ لِّلشَّـٰرِبِينَ ﴿٤٦﴾

37:46 Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.

لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ ﴿٤٧﴾

37:47 Hakina madhara, wala hakiwaleweshi.

وَعِندَهُمْ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ عِينٌ ﴿٤٨﴾

37:48 Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri.

كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ ﴿٤٩﴾

37:49 Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika.

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ ﴿٥٠﴾

37:50 Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe.

قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّى كَانَ لِى قَرِينٌ ﴿٥١﴾

37:51 Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki

يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُصَدِّقِينَ ﴿٥٢﴾

37:52 Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki

أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ ﴿٥٣﴾

37:53 Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa?

قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ ﴿٥٤﴾

37:54 Atasema: Je! Nyie mnawaona?

فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِى سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ ﴿٥٥﴾

37:55 Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.

قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ ﴿٥٦﴾

37:56 Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza.

وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّى لَكُنتُ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ ﴿٥٧﴾

37:57 Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa.

أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ ﴿٥٨﴾

37:58 Je! Sisi hatutakufa,

إِلَّا مَوْتَتَنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿٥٩﴾

37:59 Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa.

إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ ﴿٦٠﴾

37:60 Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa.

لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ ٱلْعَـٰمِلُونَ ﴿٦١﴾

37:61 Kwa mfano wa haya nawatende watendao.

أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ ﴿٦٢﴾

37:62 Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum?

إِنَّا جَعَلْنَـٰهَا فِتْنَةً لِّلظَّـٰلِمِينَ ﴿٦٣﴾

37:63 Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu.

إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِىٓ أَصْلِ ٱلْجَحِيمِ ﴿٦٤﴾

37:64 Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu.

طَلْعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَـٰطِينِ ﴿٦٥﴾

37:65 Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani.

فَإِنَّهُمْ لَـَٔاكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِـُٔونَ مِنْهَا ٱلْبُطُونَ ﴿٦٦﴾

37:66 Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo.

ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ ﴿٦٧﴾

37:67 Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka.

ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى ٱلْجَحِيمِ ﴿٦٨﴾

37:68 Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu.

إِنَّهُمْ أَلْفَوْا۟ ءَابَآءَهُمْ ضَآلِّينَ ﴿٦٩﴾

37:69 Hakika waliwakuta baba zao wamepotea.

فَهُمْ عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِمْ يُهْرَعُونَ ﴿٧٠﴾

37:70 Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.

وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ ٱلْأَوَّلِينَ ﴿٧١﴾

37:71 Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani.

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ ﴿٧٢﴾

37:72 Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.

فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُنذَرِينَ ﴿٧٣﴾

37:73 Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa.

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ ﴿٧٤﴾

37:74 Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.

وَلَقَدْ نَادَىٰنَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ ٱلْمُجِيبُونَ ﴿٧٥﴾

37:75 Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.

وَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ ﴿٧٦﴾

37:76 Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.

وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلْبَاقِينَ ﴿٧٧﴾

37:77 Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia.

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ ﴿٧٨﴾

37:78 Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye.

سَلَـٰمٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِى ٱلْعَـٰلَمِينَ ﴿٧٩﴾

37:79 Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ ﴿٨٠﴾

37:80 Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.

إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ ﴿٨١﴾

37:81 Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.

ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ ﴿٨٢﴾

37:82 Kisha tukawazamisha wale wengine.

۞ وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبْرَٰهِيمَ ﴿٨٣﴾

37:83 Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake,

إِذْ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٤﴾

37:84 Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَاذَا تَعْبُدُونَ ﴿٨٥﴾

37:85 Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?

أَئِفْكًا ءَالِهَةً دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ ﴿٨٦﴾

37:86 Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?

فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ﴿٨٧﴾

37:87 Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?

فَنَظَرَ نَظْرَةً فِى ٱلنُّجُومِ ﴿٨٨﴾

37:88 Kisha akapiga jicho kutazama nyota.

فَقَالَ إِنِّى سَقِيمٌ ﴿٨٩﴾

37:89 Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!

فَتَوَلَّوْا۟ عَنْهُ مُدْبِرِينَ ﴿٩٠﴾

37:90 Nao wakamwacha, wakampa kisogo.

فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ﴿٩١﴾

37:91 Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?

مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ ﴿٩٢﴾

37:92 Mna nini hata hamsemi?

فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًۢا بِٱلْيَمِينِ ﴿٩٣﴾

37:93 Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia.

فَأَقْبَلُوٓا۟ إِلَيْهِ يَزِفُّونَ ﴿٩٤﴾

37:94 Basi wakamjia upesi upesi.

قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ ﴿٩٥﴾

37:95 Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe?

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾

37:96 Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya!

قَالُوا۟ ٱبْنُوا۟ لَهُۥ بُنْيَـٰنًا فَأَلْقُوهُ فِى ٱلْجَحِيمِ ﴿٩٧﴾

37:97 Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!

فَأَرَادُوا۟ بِهِۦ كَيْدًا فَجَعَلْنَـٰهُمُ ٱلْأَسْفَلِينَ ﴿٩٨﴾

37:98 Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini.

وَقَالَ إِنِّى ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّى سَيَهْدِينِ ﴿٩٩﴾

37:99 Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.

رَبِّ هَبْ لِى مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ ﴿١٠٠﴾

37:100 Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.

فَبَشَّرْنَـٰهُ بِغُلَـٰمٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾

37:101 Basi tukambashiria mwana aliye mpole.

فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعْىَ قَالَ يَـٰبُنَىَّ إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلْمَنَامِ أَنِّىٓ أَذْبَحُكَ فَٱنظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَـٰٓأَبَتِ ٱفْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ ﴿١٠٢﴾

37:102 Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.

فَلَمَّآ أَسْلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾

37:103 Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.

وَنَـٰدَيْنَـٰهُ أَن يَـٰٓإِبْرَٰهِيمُ ﴿١٠٤﴾

37:104 Tulimwita: Ewe Ibrahim!

قَدْ صَدَّقْتَ ٱلرُّءْيَآ ۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ ﴿١٠٥﴾

37:105 Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema.

إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْبَلَـٰٓؤُا۟ ٱلْمُبِينُ ﴿١٠٦﴾

37:106 Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri.

وَفَدَيْنَـٰهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ ﴿١٠٧﴾

37:107 Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ ﴿١٠٨﴾

37:108 Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye.

سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ ﴿١٠٩﴾

37:109 Iwe salama kwa Ibrahim!

كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ ﴿١١٠﴾

37:110 Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.

إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ ﴿١١١﴾

37:111 Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.

وَبَشَّرْنَـٰهُ بِإِسْحَـٰقَ نَبِيًّا مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ ﴿١١٢﴾

37:112 Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema.

وَبَـٰرَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰٓ إِسْحَـٰقَ ۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ مُبِينٌ ﴿١١٣﴾

37:113 Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.

وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ ﴿١١٤﴾

37:114 Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.

وَنَجَّيْنَـٰهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ ﴿١١٥﴾

37:115 Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa.

وَنَصَرْنَـٰهُمْ فَكَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَـٰلِبِينَ ﴿١١٦﴾

37:116 Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.

وَءَاتَيْنَـٰهُمَا ٱلْكِتَـٰبَ ٱلْمُسْتَبِينَ ﴿١١٧﴾

37:117 Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha.

وَهَدَيْنَـٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ ﴿١١٨﴾

37:118 Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ ﴿١١٩﴾

37:119 Na tukawaachia (sifa njema) katika watu walio kuja baadaye.

سَلَـٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ ﴿١٢٠﴾

37:120 Iwe salama kwa Musa na Haruni!

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ ﴿١٢١﴾

37:121 Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.

إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ ﴿١٢٢﴾

37:122 Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini.

وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ ﴿١٢٣﴾

37:123 Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.

إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٢٤﴾

37:124 Alipo waambia watu wake: Hamwogopi?

أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ ٱلْخَـٰلِقِينَ ﴿١٢٥﴾

37:125 Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,

ٱللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ ﴿١٢٦﴾

37:126 Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?

فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٢٧﴾

37:127 Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ ﴿١٢٨﴾

37:128 Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ ﴿١٢٩﴾

37:129 Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye.

سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِلْ يَاسِينَ ﴿١٣٠﴾

37:130 Iwe salama kwa Ilyas.

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ ﴿١٣١﴾

37:131 Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.

إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾

37:132 Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.

وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٣﴾

37:133 Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.

إِذْ نَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ أَجْمَعِينَ ﴿١٣٤﴾

37:134 Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,

إِلَّا عَجُوزًا فِى ٱلْغَـٰبِرِينَ ﴿١٣٥﴾

37:135 Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma.

ثُمَّ دَمَّرْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ ﴿١٣٦﴾

37:136 Kisha tukawaangamiza wale wengineo.

وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ ﴿١٣٧﴾

37:137 Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,

وَبِٱلَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٣٨﴾

37:138 Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?

وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٩﴾

37:139 Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.

إِذْ أَبَقَ إِلَى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ ﴿١٤٠﴾

37:140 Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.

فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُدْحَضِينَ ﴿١٤١﴾

37:141 Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa.

فَٱلْتَقَمَهُ ٱلْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿١٤٢﴾

37:142 Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.

فَلَوْلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾

37:143 Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,

لَلَبِثَ فِى بَطْنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾

37:144 Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.

۞ فَنَبَذْنَـٰهُ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٌ ﴿١٤٥﴾

37:145 Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.

وَأَنۢبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ ﴿١٤٦﴾

37:146 Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye.

وَأَرْسَلْنَـٰهُ إِلَىٰ مِا۟ئَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ ﴿١٤٧﴾

37:147 Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.

فَـَٔامَنُوا۟ فَمَتَّعْنَـٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍ ﴿١٤٨﴾

37:148 Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.

فَٱسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ ٱلْبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلْبَنُونَ ﴿١٤٩﴾

37:149 Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?

أَمْ خَلَقْنَا ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ إِنَـٰثًا وَهُمْ شَـٰهِدُونَ ﴿١٥٠﴾

37:150 Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?

أَلَآ إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ ﴿١٥١﴾

37:151 Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:

وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ ﴿١٥٢﴾

37:152 Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!

أَصْطَفَى ٱلْبَنَاتِ عَلَى ٱلْبَنِينَ ﴿١٥٣﴾

37:153 Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?

مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿١٥٤﴾

37:154 Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?

أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٥﴾

37:155 Hamkumbuki?

أَمْ لَكُمْ سُلْطَـٰنٌ مُّبِينٌ ﴿١٥٦﴾

37:156 Au mnayo hoja iliyo wazi?

فَأْتُوا۟ بِكِتَـٰبِكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ ﴿١٥٧﴾

37:157 Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.

وَجَعَلُوا۟ بَيْنَهُۥ وَبَيْنَ ٱلْجِنَّةِ نَسَبًا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ ٱلْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٥٨﴾

37:158 Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.

سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٥٩﴾

37:159 Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia.

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٠﴾

37:160 Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.

فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ ﴿١٦١﴾

37:161 Basi hakika nyinyi na mnao waabudu

مَآ أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَـٰتِنِينَ ﴿١٦٢﴾

37:162 Hamwezi kuwapoteza

إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ ٱلْجَحِيمِ ﴿١٦٣﴾

37:163 Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni.

وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ ﴿١٦٤﴾

37:164 Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.

وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلصَّآفُّونَ ﴿١٦٥﴾

37:165 Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.

وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلْمُسَبِّحُونَ ﴿١٦٦﴾

37:166 Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.

وَإِن كَانُوا۟ لَيَقُولُونَ ﴿١٦٧﴾

37:167 Na walikuwapo walio kuwa wakisema:

لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ ﴿١٦٨﴾

37:168 Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,

لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٩﴾

37:169 Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi.

فَكَفَرُوا۟ بِهِۦ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿١٧٠﴾

37:170 Lakini waliukataa. Basi watakuja jua.

وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلْمُرْسَلِينَ ﴿١٧١﴾

37:171 Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa.

إِنَّهُمْ لَهُمُ ٱلْمَنصُورُونَ ﴿١٧٢﴾

37:172 Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ ﴿١٧٣﴾

37:173 Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.

فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٤﴾

37:174 Basi waachilie mbali kwa muda.

وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٥﴾

37:175 Na watazame, nao wataona.

أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ ﴿١٧٦﴾

37:176 Je! Wanaihimiza adhabu yetu?

فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلْمُنذَرِينَ ﴿١٧٧﴾

37:177 Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa.

وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٨﴾

37:178 Na waache kwa muda.

وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٩﴾

37:179 Na tazama, na wao wataona.

سُبْحَـٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٨٠﴾

37:180 Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia.

وَسَلَـٰمٌ عَلَى ٱلْمُرْسَلِينَ ﴿١٨١﴾

37:181 Na Salamu juu ya Mitume.

وَٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ﴿١٨٢﴾

37:182 Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Jipime

Jipime →

Hear Surah As-Saffat from all 90 reciters →