بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيْتُونِ ﴿١﴾
95:1 Naapa kwa tini na zaituni!
وَطُورِ سِينِينَ ﴿٢﴾
95:2 Na kwa Mlima wa Sinai!
وَهَـٰذَا ٱلْبَلَدِ ٱلْأَمِينِ ﴿٣﴾
95:3 Na kwa mji huu wenye amani!
لَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ فِىٓ أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾
95:4 Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
ثُمَّ رَدَدْنَـٰهُ أَسْفَلَ سَـٰفِلِينَ ﴿٥﴾
95:5 Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٦﴾
95:6 Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.
فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِٱلدِّينِ ﴿٧﴾
95:7 Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
أَلَيْسَ ٱللَّهُ بِأَحْكَمِ ٱلْحَـٰكِمِينَ ﴿٨﴾
95:8 Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?